ENZI ZANGU KIJANA


By: Saul Kalivubha.

Nilipendwa na warembo, kijana nikapendeka,

ngesema nina  urimbo, kwa kweli niliwateka,

sikuwahi kwenda kombo, mitego iliteguka,

Enzi zangu za ujana, imebaki kumbukizi.

 

Kijana mtanashati, ni nani hakunijua?

kijana wa kisimati, mabinti walisifia,

Nalijiona bahati, ujana kufurahia,

Sasa sina nguvu tena, fainali uzeeni.

 

Sasa sina nguvu tena, warembo kuwapupia,

Ngozi  imekunjamana, naita wanakimbia,

sina tena umaana,kutembea naguchia,

Siku nazirudi nyuma, ujana unirudie.

 

Kadi tama sina budi, kalamu naweka chini,

uzee nina kaidi, unanijaza huzuni,

rudi tena ikibidi, nitese kama zamani,

Ujana umeniacha, ingali nakuhitaji.

Previous Facts about butterflies
Next PARENTS OF (KCPE) 2020 CANDIDATES HAVE BEGUN PRESSURING SECONDARY SCHOOL PRINCIPALS FOLLOWING DELAYS IN FORM ONE PLACEMENTS.

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *