NGUVU SIZIDI AKILI


By: Linus Siwiti linussiwiti12@gmail.com

Jambo moja nimewaza, la muhimu tena sana,

Kwa tungo nakueleza, si yahaba ni mapana,

Tulia na sikiliza, gonjwa uweze kupona,

Nguvu sizidi akili, vizuri  ukifikiri.

 

  1. Vizuri ukifikiri, nguvu kidogo tumia,

Ukweli ninaukiri, usije ukaumia

Pata muda tafakari, ya utopia zuia,

Nguvu sizidi akili, mawazo pima vizuri.

 

  1. Mawazo pima vizuri, inafaida dawamu,

Pokea hizi habari, kusoma uone hamu,

Maisha yatafakari, jipatie ufahamu,

Nguvu sizidi akili, maarifa zingatia.

 

  1. Maarifa zingatia, vitabu kiweza soma,

Vingi utafurahia, uanze

bado mapema,

Mbeleni utajutia, simama sasa simama,

Nguvu sizidi akili, ujumbe nimefikisha

 

  1. Ujumbe nimefikisha, ukingoni nimefika,

Tano nazikamilisha, amka vema amka

Soma vya kuelimisha, ubongo pate shituka,

Nguvu sizidi akili, kadawamu utasota.

Previous Mishandling of currency notes blamed for quick wear and tear
Next Bar owners plead for more operating hours

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *