Shairi: Sitachoka kukupenda


1 Subiri nikuambie, kilichonivuta kwako

Siri ni ikuibie,     hakuna zaidi  yako

Mola atukabalie,  daima niwe wakwako

Sitachoka kukupenda

 

2  Upole tabia yako,   napenda yako maringo

Ucheshi  hulka yako, na hauna songombingo

Laini sauti yako,  yanituliza ubongo

Sitachoka kukupenda

 

3 Kwenye kosa nisamehe,  tuishi hadi kiyama

Tamu zaidi ya kuhe, penzi halitosimama

Una umbo la kihehe, twende akuone Mama

Sitachoka kukupenda

 

4 Nitaizuru dunia, nikisema lako jina

Moyoni ninaumia, muhibu  unaponuna

Nakupenda wangu dia, pendo ni kubwa amana

Sitachoka kukupenda

 

©️ Abuuabdillah✍️

0744883353

jumaomari5@gmail.com

Kilimanjaro🇹🇿

Previous Colleen Mapatwana
Next Lawyers make their case against BBI ruling

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *